Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wanafunzi wa Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) – Dar-es-salaam, Tanzania, wakiendelea na Mibahatha yao ya Kisayansi na Utafiti mbalimbali katika Maktaba ya Chuo hiki.
Mubahatha na Utafiti wa Kielimu ni moyo wa Elimu ya Kiislamu. Kupitia mijadala ya kielimu, Wanafunzi hubadilishana maarifa, kufungua milango ya utafiti, na kuimarisha uelewa wa kina wa masomo yao.
Ukweli ni kwamba: Elimu bila Mubahatha ni kama mwili bila roho. Hupotea taratibu, na haidumu katika fikra za Mwanafunzi.
Hivyo basi, kusoma haimaanishi kusikiliza au kusoma vitabu pekee – bali pia ni kushiriki kikamilifu katika mijadala, kuuliza maswali, na kutafuta majibu ya kielimu kwa pamoja.
Tuimarishe elimu yetu kwa moyo wa utafiti na mijadala ya kielimu.
Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Nguzo ya Malezi ya Kielimu na Kiroho.
Your Comment